
Klabu ya Yanga ilifanya mazoezi yake ya mwisho jana jioni kwenye
uwanja wa Essipong Sports mjini Sekondi, Ghana kwa ajili ya mchezo
wao wa marudiano dhidi ya Medeama utakaochezwa leo Jumanne Julai 26.
Yanga ililazimishwa sare
ya kufungana bao 1-1 na Medeama kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa taifa
takribani juma moja lililopita na kupata pointi ya kwanza katika mechi zake
tatu ilizocheza.
Mabingwa hao wa Tanzania wanashika nafasi ya mwisho katika Kundi
A hivyo watakuwa na kibarua kizito cha kutafuta ushindi ugenini katika mchezo
wao wa nne katika hatua ya makundi.
Yanga iliondoka nchini
siku ya Jumamosi Julai 23 kuelekea Ghana kupambana kuhakikisha inapata pointi
tatu kwa mara ya kwanza tangu ilipofuzu kwenye hatua ya makundi kombe la
shirikisho Afrika.
Post a Comment