SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: BAADA YA KUTWAA MEDALI INDIA, SIMBU APEWA JUKUMU JINGINE TENA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
BAADA ya Alphonce Simbu kufanya vyema kwenye mashindano ya mbio za Mumbai Marathon, sasa chama cha riadha Tanzania, RT chamkabidhi m...
20170115_164632

BAADA ya Alphonce Simbu kufanya vyema kwenye mashindano ya mbio za Mumbai Marathon, sasa chama cha riadha Tanzania, RT chamkabidhi majukumu mengine.

Simbu ambaye kwenye mbio hizo alifanikiwa kushika nafasi ya kwanza na kuondoka na medali pamoja na kitita cha dola 67,000 ambazo ni sawa na Sh milioni 147 za Kitanzania, Agosti mwaka huu anatarajiwa kushiriki mbio za World Athletic Championship zitakazofanyika London, England.

Katibu Mkuu wa RT, Wilhelm Gidabuday, ameliambia Championi Jumatano kuwa: “Fedha alizopata zimegawanyika sehemu tatu na kufikia hizo dola 67,000, zawadi za mshindi wa kwanza ni dola 42,000, lakini kutokana na kufanya kwake vizuri kwenye Olimpiki alipata mwaliko maalum ambao ulikuwa na kipengele kwamba akishinda au akishindwa lazima apewe dola 15,000 na wastani mzuri wa kukimbia akapata bonasi ya dola 10,000.

“Kilichobaki sasa tunataka aende London kwenye mashindano ya World Athletic Championship na kurudi na medali, tukipata medali huko ni heshima kubwa kwani haya ni ya pili kwa ukubwa ukiondoa Olimpiki.”


Chanzo; Champion.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top