
BAADA
ya kukaa kimya kwa muda mrefu, aliyekuwa kocha wa zamani wa klabu ya Manchester
United, Loius Van Gaal, ameibuka na kukanusha taarifa zilizokuwa zikisambaa ya
kuwa amestaafu kufundhisha maswala ya soka.
Van Gaal amekuwa nje ya
uwanja tangu atimuliwe na mabosi wa Manchester United mwezi May mwaka jana.
Jumatatu hii gazeti
moja la Uholanzi De Telegraaf lililipoti ya kwamba Van Gaal amestaafu
kufundisha soka sababu kubwa ikiwa ni kufiwa na mjukuu nwake.
Lakini akifanya
mahojiano na kituo kimoja cha redio Cadena Ser, nchini Hispania, Van Gaal amesema japo mswala la kustaafu
linawezakana, lakini bado halijafahamika.
Vilevile, Mholanzi huyo alitanabaisha kuikacha ofa ya klabu ya Valencia
walipomtaka kuwa kocha wao mkuu.
“Kama nitaendelea au la, itategemea na ofa nitakazozipata” Alisema Van
Gaal.
“Nimefundisha klabu nyingi hapa barani ulaya lakini nahisi nimekuwa sina
maendeleo mazuri nikiwa kwenye ngazi ya vilabu”
“Siwezi kustaafu kwa muda huu, lakini nitaamua mwishoni mwa likizo yangu
ambayo inaishia mwezi June au July”
Van Gaal ameshinda mataji 7 akiwa na vilabu mbalimbali kama vile AZ,
Barcelona, Bayern n.k kabla hajaihamia Manchester United.
Post a Comment