
Mkufunzi wa mabingwa wa
EPL, Claudio Ranieri amesema kuondoka kwa Kiungo wao Ngolo Kante hakuna haja ya
kuthibitisha ya kuwa litakuwa pengo kubwa sana. Meneja wa Mbweha hao wa
jangwani, amesema ana matumaini kutakuwa hakuna tena kupoteza kwa kuuza
mchezaji na kuongeza ya kuwa hela zipo kwaajili ya kuboresha kikosi chao.
Kiungo mchezeshaji, raia
wa Ufaransa, alikuwa anatumika katika kikosi hicho katika nafasi tofauti na
kuisaidia Leicester kutwaa kombe la EPL msimu uliomalizika.
Kante 25 ameuzwa katika
klabu ya Chelsea lakini mkufunzi wa klabu hiyo Ranieri amesema yuko bize
kuhakikisha anafukia shimo lililoachwa na Kante aliyekuwa na umuhimu mkubwa
klabuni hapo.
‘‘Nafikiri ni vilevile
tu kama ilivyokuwa mwanzo tukiwa na Cambiasso” Alisema Ranieri. ‘‘Ilikuwa ni
ngumu kupata mbadala wake, lakini tayari tumekwisha kamilisha, ni vilevile, tu,
soccer linaendelea, hakuna kusimama”

‘‘Mpira unaweza ukanipotea
mimi Wes [Nahodha wa mbweha], mtu yeyote lakini pia bado watu wakaendelea kucheza
mpira huohuo, nafikiri tuna kikosi bora sana na subiri tuone, kama kuna kitu
kingine cha ziada tutakuwa tunakihitaji, bosi wetu yupo tayari kununua”
Ranieri alikuwa
akiyaongea haya kuelekea mchezo wao dhidi ya PSG katika kombe la ICC huko
nchini China pamoja na Marekani na Austria. Na Leicester walikuwa wanapewa
nguvu lakini pia Andy King kuweza kufuata nyayo za Jamy Vardy kwa kuweza
kusaini mkataba mrefu kuwa klabuni hapo.

Ranieri pia amesema
anatumai wachezaji wengine muhimu wa kikosi hicho kama vile golikipa Kasper Schmeichel pamoja na fowadi Riyad
Mahrez wataendelea kuwepo kikosini hapo.
‘‘Klabu inafanya vizuri sana, nafikiri wanataka kubaki nasisi, kujaribu
na kuboreka kila kukicha kama msimu uliopita ni vigumu sana, lakini tutakuwa
bora” Alisema Ranieri.
‘‘Ni jambo la muhimu wamesaini na kubaki nasisi kuendeleza maisha ya
Leicester wakiwa kama mabingwa na subiri tu tuone itakavyokuwa” Alimalizia
Ranieri.
Post a Comment