.
Mkurugenzi wa klabu ya
FC Wolfsburg amesema mchezaji wao Julian Draxler ataendelea kubaki klabuni hapo
kwa misimu mingine Zaidi mpaka hapo watakapoamua kumuuza klabu nyingine.
Klabu ya Asernal ya
nchini England imekuwa inahusishwa juu ya kutaka kumsajili mchezaji huyo ambae
alikuwa sehemu ya kikosi cha ujerumani kilichotolewa katika hatua ya nusu
fainali ya mataifa ya ulaya, mashindano yaliyofanyika nchini ufaransa na timu
ya taifa ya ureno kutawazwa mabingwa.
Lakini Allofs amesisitiza
ya kuwa hawawezi kumuuza Draxler na kuweza kutanabaisha ya kuwa huenda
aliyekuwa mchezaji wa klabu ya Chelsea Andre Schurrle akaihama klabu hiyo.
‘‘Kwa Julian
Draxler, ni asilimia 100 ya kuwa hataondoka na hakutakuwa na mjadala Zaidi”
Alieleza Allofs.
Wolfsburg wangependa
kumwona Shurrle akiendelea kukua chini yao, lakini tetesi kutoka klabu ya
Borussia Dotimund zimewafanya waweze kumwachia Shurrle afanye mazungumzo nao na
endapo watakubaliana nae basi watamwachia aende zake.
Shurrle amemwambia
mkufunzi wake ya kuwa Borussia Dotimund imemfanya aifikirie mara mbili na
huenda akafanya maamuzi ya kuisaini klabu hiyo.
Draxler ana msimu mmoja
klabuni Wolfsburg tangu ajiunge nao akitokea shakle wakati Shurrle alijiunga na
klabu hiyo mwaka jana akitokea klabu ya Chelsea.
Post a Comment