Amesukuma
gozi mara 143 akiwa na timu ya Palacena kufanikiwa kufunga magoli kumi na tatu,
na baadaye akabadilika na kuwa kiungo mbadala katika mechi ya mwishoni mwa wiki
iliyopita pale timu yake ilipofungwa na West Brom bao moja kwa nunge.
Meneja wa timu ya Palace Alan Pardew alisema
baada ya kufungwa bao moja kwa yai tulitambua kuwa moyo na nafsi yake ziko viko
mahali kwingine
Bolasie anasema kwamba uamuzi wa kuhamia upande
wa Mersey haukuwa wa busara na kuongeza kwamba lakini sasa nimeibukia Everton,
kazi haijafanyika bado Napaswa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa na kujisikia
nimo ndani yake. “Niko tayari kukabiliana na changamoto zilizoko mbele yangu, sio
suala la pesa kwa upande wangu, suala ni kutimiza malengo ya baadaye ya klabu
na kule ambako wanatarajia kuifikisha, napenda tu kucheza mpira”
Naye meneja wa timu ya Everton Ronald Koeman
anasema kwamba mchezaji huyo Yannick ni mchezaji aliyekuwa anamnyemelea muda
mrefu ulio pita kwasababu ni aina ya winga anaye mpenda, kwanza ana kasi, ana
nguvu, na anao uwezo mkubwa wa kucheza katika nafasi mbali mbali hasa mstari wa
mbele.
Bolasie
ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Everton katika majira haya ya kiangazi.
Moja ya majembe hayo yaliyosajiliwa ni pamoja
na mlinda mlango Maarten Stekelenburg anatokea timu ya Fulham, Idrissa Gueye
kutoka Aston Villa, wakati kiongozi wa timu ya Wales Ashley Williams aliungana
na timu hiyo tarehe kumi ya mwezi huu akitokea Swansea kwa ada isiyojulikana,
huku ikidhaniwa kuwa ni paundi milioni kumi na mbili.
Everton, ilitoka sare ya goli 1-1 mwishoni mwa
juma lililopita na timu ya Tottenham, wako kwenye mazungumzo ya kumsajili beki
wa Sunderland Lamine Kone huku nia ikiwa wazi ya kusalia na mshambuliaji Romelu
Lukaku.
Aidha, mfanya biashara mkubwa kutoka nchini
Irani Farhad Moshiri amenunua hisa asilimia 49.9 % katika timu ya Everton mapema
mwaka huu mnamo mwezi wa pili, na kuhitimisha ukame wa muongo mzima wa kusaka
uwekezaji mpya.
Post a Comment