SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: RONALDO, BALE NA GREEZMAN. NI NANI ATAKUWA MCHEZAJI BORA WA ULAYA?
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
NYOTA wawili wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale watapambana na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid kuwania tuzo ya M...



NYOTA wawili wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale watapambana na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Ulaya.

Bodi ya Soka Ulaya (UEFA) imetangaza orodha fupi ya mwisho ya wachezaji watatu wa kuwania tuzo hiyo leo na wachezaji wa la Liga watupu watachuana, tena wote kutoka timu za Jiji la Madrid.

Mshindi wa tuzo hiyo atapatikana baada ya kupigiwa kura na matokeo yatatangazwa katika Grimaldi Forum mjini Monaco Agousti 25.

Waandishi wa Habari kutoka nchi zote wanachama 55 wa UEFA watawasilisha orodha yao fupi, huku 54 wakipiga kura.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top