
Wekundu wa
Msimbazi Simba SC baada mfululizo wa matokeo mazuri katika mechi zao za
kirafiki, leo wakajikuta wakilala bao 1-0 kutoka kwa timu ya Halmashauri ya
Wilaya ya Kinondoni KMC, mchezo ulifanyika mkoani Morogoro.
KMC walipata bao pekee katika mchezo wa jana kupitia kwa
Rashidi Roshwa mnamo dakika ya 10 kufuatia kazi nzuri iliyofanywa na Emanuel
Memba.
Simba, ambayo jana safu yake ya ushambuliaji ilikuwa
ikiongozwa na Ame Ally ‘Zungu’ aliyetokea Azam kwa mkopo walikosa nafasi nyingi
za wazi ambazo pengine zingeweza kubadili matokeo ya mchezo.
Simba wanatarajiwa kurejea jijini Dar es Salaam kati ya leo
au kesho tayari kujiandaa na mchezo dhidi ya ya FC Leorpads ya Kenya kuelekea
siku ya maadhimisho ya Simba day, ambapo kilele chake ni Agosti 8.
Post a Comment