SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: UTABIRI WA DR. LEAKY, MANCHESTER CITY BINGWA MZEE WENGER ATAFUKUZWA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mchambuzi wa masuala ya soka mahiri nchini Tanzania Dr. Leaky ametoa utabiri wake ya kuwa klabu ya Manchester City ya nchini England nd...

Mchambuzi wa masuala ya soka mahiri nchini Tanzania Dr. Leaky ametoa utabiri wake ya kuwa klabu ya Manchester City ya nchini England ndiyo itakuwa bingwa wa msimu wa ligi kuu wa mwaka 2016-2017.
Dr Leaky ambaye tunatarajia kumwona katika simu za karibuni kwenye kituo cha televisheni cha TV1, stesheni ambayo imepewa majukumu ya kuonyesha ligi ya EPL msimu huu, ameyaongea hayo huku akifafanua ya kuwa kwa sababu ya usajili mzuri alioufanya Pep Guardiola, basi anafikiri kwamba Guardiola ndiye atakayeibuka kidedea wa mbio hizo zinazotarajiwa kuanza rasmi tarehe 13 mwezi huu.
‘‘Katika miaka ya karibuni hakuna amekuwa na kazi ngumu kama mtabiri wa hali ya hewa Kuna siku zilizopita hapa, watabiri wa hali ya hewa wote waliomba kuacha kazi, kwa sababu walipokuwa wakitabiri, yalikuwa yakifanyika vingine kama uligundua” Alisema Dr. Leaky.
‘‘Kila mara mambo yamekuwa yakienda kinyume, anayeweza kutabiri sasa hivi mapema ligi ya Wingereza itakuwaje, anataka kweli awe ni mtu mwenye roho ngumu, Lakini na mimi nina roho ngumu, naweza nikakwambia mwaka huu bingwa nafikiri, atakuwa ni Pep Guardiola” Alisema Dr. Leaky
Alipoulizwa na jopo la waaindishi wa habari za kimichezo ni kwa nini ametupa karata yake kwa Guardiola, Dr. Leaky alisema, ‘‘Kwa mfano sasa tuseme wale watu wanaobeti, unapobeti unaangalia nini, unaangalia uwezo wa timu, unaangalia, huyu jamaa timu yake iko kiasi gani, ana wachezaji wazuri kiasi gani, yeye mwenyewe ni mzuri kiasi gani, ameongeza wachezaji wazuri kiasi gani. Kutoka katika kiwango alichokuwepo na hawa wa akina Norito ambao amewaleta, watampeleka wapi? Namwangalia MAN U kutoka alipokuwepo, na hata tukimleta Pogba na Ibrahimovic, na wote ambao amewaongeza, je atakuwa amesogea upande gani, Unajua kwa bahati mbaya MANU alikuwa ni mtu ambaye amekunywa sana, akawa anaelekea nyumbani, akawa anayumbayumba, watu wakasema huyu ataanguka tu, lakini bado yeye akawa anawaambia aaah wapi sianguki mimi naenda, badala ya kuanguka akafika akajigonga kwenye mti, akaanguka. Ndio hayohayo, Man U ilikuwa kila mtu anamwona huyu ataanguka, lakini alikuwa hajiamini anajipa matumaini, Sasa kutoka katika kile kiwango kufika mara moja kuweza kuchukua ubingwa sio rahisi.”
Na Dr. Leaky akaendelea akisema mpinzani pekee wa ManCity atakuwa ni Chelsea. Lakini alipoulizwa kwa upande wa Arsenal, Dr. Leaky akasema mzee Wenger huu ndio mwaka wake wa mwisho.
‘‘Timu yangu sitaki kusema, lakini kuna wengine ambao nafikiri utabiri wangu mwingine unataka, Mzee Arsene Wenger ni mwisho msimu huu. Ama watamtoa watu kwa vile vigali vya Kariakoo vinavyobeba mizigo, basi vile vya namna ile ndivyo vilivyombeba Van Gaal. Basi vile vya namna ile vitambeba pia Wenger ama yeye atakataa kuifundisha timu yeye.”
Na Dr. Leaky akahitimisha akisema, ‘‘kwa hiyo utabiri wangu, bingwa Guardiola, Mzee Wenger huu ndio msimu wake wa mwisho.” Alimaliza Dr. Leaky.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top