.jpg)
MWEZI
Agosti 14 ya mwaka huu, Shirikisho La Mpira wa miguu mkoa wa Kagera lilifanya
uchaguzi wa mkoa huo na kumpitisha Rais wa TFF, Jamal Emily Malinzi kuwa
mwenyekiti wa KRFA kwa ushindi wa kura 21 kati ya kura 22 zilzopigwa.
Malinzi umefanya
maamuzi magumu ambao kila mdau wa mpira anatamani kujua nini haswa
kilichokusukuma ukaamua kugombea nafasi ya uwenyekiti ili hali ukiwa bado ni
rais wa shirikisho la mpira wa miguu nchini TFF.
Umeamua kuvaa kofia
mbili, moja kichwani na nyingine umeivalisha kwenye mgumi ya mkono wako wa
kushoto, sehemu ambayo mimi nakukumbusha sio eneo stahiki zaidi ya lile la
kichwani ambapo tayari ulishavaa kofia ile ya kwanza.
Nafahamu ni macho ndio
yaliyokuvutia kununua kofia zote mbili ambazo sasa kwa tamaa ya kuvaa ili
upendeze, inakushawishi uvae zote kwa wakati mmoja jambo ambalo pengine unaweza
ukawa ni wa kwanza kulifanya tangu dunia hii iumbwe.
Labda nikukumbushe kama
ulikuwa umesahau, kabla ya kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa KRFA, Malinzi ulikuwa
na bado mpaka sasa ni rais wa shirikisho la mpira wa miguu Nchini TFF,
Ulizipitia kanuni na
sheria za Baraza la Michezo la Taifa lakini hata zile za TFF? Bila shaka
unazifahamum sema umeamua kufunga vioo vya gari ili ututimlie vumbi sie tusio
na hatia.
Kwa mujibu wa kanuni na
taratibu za uongozi za BMT, Malinzi haukustahili hilo ulilolifanya Agosti 14.
Sheria ya Baraza la
Michezo la Taifa Na. 12 ya 1967 na
marekebisho yake ya Na. 6 ya 1971 pamoja na kanuni za BMT na kanuni za usajili
za 1999, 8[1] zinasema,
“Mwenyekiti, Mkamu mwenyekiti,
Katibu mkuu, Katibu msaidizi na Mweka hazina wa chama cha mchezo wowote
hatoruhusiwa kushika nafasi ya uongozi zaidi ya moja kwenye vyama tofauti
vinavyoshughulikia aina moja ya mchezo”
Lakini umebariki kura
za wajumbe wa mkoa wa Kagera lakini pia ukiwa bado ni rais wa shilikisho la mpira
wa miguu Tanzania, au kuna utofauti wa aina ya michezo kati ya TFF na KRFA?
Hapo Malinzi umetuweka wengi kwenye mabano tusijue hata wapi tutatokea.
Aidha katika kifungu
cha 8, kifungu kidogo cha 2 cha sheria hiyo kinasema,
“Endapo viongozi
waliotajwa katika kanuni ya 8 [1] watagombea na kupata uongozi kwenye ngazi
nyingine ya chama cha mchezo huo huo, Watalazimika kuachia nafasi moja ya
uongozi waliyokuwa wakishikilia na kubaki na moja tu”
Wakati mwingine, huu
tunaiuita uchu wa madaraka kama bado hauna ndoto ya kuiuza kofia moja ili ubaki
na ile moja uliyoivaa kichwani na ile ya kwenye ngumi ya mkono wa kushoto,
waachie wengine watakaoona inawafaa.
Lakini umekaa kimya,
kama vile hakuna kinachoendelea ndani ya mpira wa miguu nchini, na hata lile
sakata la klabu ya Stand United umeona haina maana ila umeanzisha lako ambalo
pengine ni la makusudi kwani kila kitu unakifahamu.
Mathalani, ukiwa kama
mwenyekiti wa KRFA lakini pia ukiwa kama rais wa TFF, likiwa limetokea jambo la
kusimama kama mwemyekiti wa mkoa kwa upande wa taifa ambako ndio unamkuta TFF,
hapo limekaaje Malimzi?
Au, mfano mwingine wa
kawaida sana, ile ishu ya Polisi Tabora na Mwadui FC. Kama moja ya timu hizi
ingekuwa Kagera, kivuli cha mwenyekiti mkoa angesimama nani na kule upande wa
TFF angekuwa nani? Hauoni hapo kunavyokuwa na mgongano wa maslahi?
Maamuzi yako
yamepelekea watu kufikiri kila walichokifikiria na hata kuirudisha siasa ndani
ya mpira wa miguu jamba ambalo nilikuwa nafikiri kuwa limeisha sasa kumbe kiongozi mkubwa kama wewe unaamua
kuirudisha tena.
Kuna haja gani ya
kulilia mabadiliko kwenye michezo kama viongozi ndio wanaoongoza kwa kutengua
sheria na kanuni zilizowekwa na baraza linalosimamia michezo nchini.
Hakiki umekuwa kinyume
na matarajio ya wengi wanaotaka mabadilikoa na wewe mwenzetu ukiwa kama
kiongozi hilo wala hujali kwani tayari hesabu zako za darasa la sita
zilikwishatimia.
Yakupasa usimame kwa
miguu yako mwenyewe na utamke kwa kinywa chako kama haya tunayosema
tunakutwisha mzigo usio wako au ni sahihi tu hata ukikaa kimya.
Post a Comment