Picha na Salehe Jembe. |
BAADA ya ukarabati wa
miaka mitatu wa uwanja wa uhuru, maarufu kama shamba la bibi, na wakandarasi
wachina, leo uwanja huo umekabidhiwa mikononi mwa serikali.
Kampuni ya Beijing Construction Engineering Group (BCEG) ya nchini China ambayo ilikuwa ikisimamia marekebisho ya uwanja huo chini ya meneja wake mkuu, Cheng Longhai, walimkabidhi Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye katika hafla fupi iliyofanyika uwanjani hapo, mapema hii leo.
Akizungumza baada ya kukabidhiwa uwanja huo Nape alisema: “Ni jambo la busara
kwa kila atakayeutumia uwanja huu kuwa mlinzi kwa mwenzake ili kulinda
miundombinu yake ili udumu kwa miaka mingi zaidi kwani hii ni hazina yetu
sote.”
Wakati huohuo, mbunifu wa michoro ya uwanja huo, Aloyse Peter Mushi, alisema: “Uwanja huu unaingiza watu waliokaa elfu 23, lakini wakikaa kwa kubanana wanafika elfu 25, tulianza marekebisho haya mwaka 2013, na tunashukuru leo hii umekamilika na serikali kukabidhiwa”

Hivyo, baada ya marekebisho hayo, uwanja
huo utatumika kwenye mechi mbalimbali, zikiwemo zile za ligi kuu VPL.
Post a Comment