
NAHODHA wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa
Stars, na mshambuliaji wa klabu ya KRC Genk, Mbwana Ally Samatta ameendelea
kufanya vyema baada ya hapo jana kuiongoza timu yake ya Genk kushinda ushindi
mujarabu wa goli 3-0 dhidi ya Lokeren.
Samatta
alianza kufunga goli la kwanza dakika ya 34 kipindi cha kwanza kabla ya kufunga
bao jingine dakika nne baadaye.
Bao
la tatu la Genk limefungwa na Leon Bailey dakika ya 48 kipindi cha pili na
magoli hayo yakidumu kwa dakika zote.
Samatta
alipumzishwa dakika ya 73 kumpisha mshambuliaji mwenye asili ya Ugiriki Nikos
Karelis.
Kwa
ushindi huyo, klabu ya Genk inapaa hadi nafasi ya nne kwa kuwa na pointi 7 kuku mbele yake zikiwepo timu kama, Zulte
Waregen, Anderlecht na Spoting Chalrelou.
.
Post a Comment