SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Wasiwasi kumhusu Hazard Euro 2016
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
      Wasiwasi kumhusu Hazard Euro 2016 Na Charles Kunji. Timu ya taifa ya Ubelgiji inasubiri kwa muda kubaini iwapo mcheza...
      Wasiwasi kumhusu Hazard Euro 2016

Hazard



Na Charles Kunji.



Timu ya taifa ya Ubelgiji inasubiri kwa muda kubaini iwapo mchezaji wao tegemezi Eden Hazard ataweza kuwachezea mechi muhimu ya Euro 2016 dhidi ya Wales siku ya Ijumaa.
Hazard, 25, mshambuliaji wa Chelsea, alifunga bao katika ushindi wao wa goli 4-0 dhidi ya Hungary katika hatua ya mtoano.
Hata hivyo, aliumia paja wakati wa mechi hiyo na hajashiriki mazoezi tangu wakati huo.
"Tunafanya kila juhudi kuhakikisha yuko asilimia 100 sawa kucheza,” amesema meneja wa Ubelgiji Marc Wilmots.
"Siwezi nikawapa hakikisho kuhusu ni wakati gani hili litafanyika, na pia siwezi nikawathibitishia kwamba atakuwa sawa.”
Vijana hao wa Wilmots, walioorodheshwa nambari mbili kwa ubora duniani, walicheza dhidi ya Wales wakati wa mechi za kufuzu kwa Euro 2016 na Kombe la Dunia 2014.
Walishindwa mechi zote tatu walizocheza karibuni zaidi.
Mechi ya karibuni zaidi Wales walishinda 1-0 mjini Cardiff Juni 2015.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top