yanga yakubali kichapo
![]() |
picha na shaffih |
Na Charles Kunji.
Hakika ngoma ya mwana haikeshi, na ushindi wa klabu ya yanga wa
kwanza katika mashindano ya shirikisho barani afrika bado ni kitendawili.
Baada ya kupoteza mechi yao ya kwanza ugenini dhidi
ya MO Bejaia ya Algeria, leo klabu ya yanga walikuwa nyumbani wakikipiga dhidi
ya TP Mazembe mchezo uliomalizika kwa Yanga kupoteza tena kwa goli 1-0.
Goli la Mazembe lilitokana na mpira wa adhabu ndogo
baada ya Kelvin Yondani kumuangusha Thomas Ulimwengu nje kidogo ya eneo la
hatari. Mpira wa adhabu ndogo ulimfikia Merveille Bope na kuupachika kambani
baada ya mabeki wa Yanga kushindwa kuuondosha kwenye eneo lao la hatari.
Tayari Yanga imeshacheza mechi mbili kwenye hatua ya
makundi, wamefungwa zote kwa goli moja huku wao wakiwa bado hawajafunga bao
hata moja katika mechi walizocheza.
Klabu ya yanga iliweza kuwatumia wachezaji wapy
waliosajiliwa kama Juma Mahadhi aliyetoka timu ya coastal union iliyoshuka daraja
na mahadhi kuonyesha mchezo wa kuvutia katika mechi yake ya kwanza ya
kimataifa.
Katika kundi A, Tp mazembe wanaongoza kundi hilo wakiwa wamecheza mechi
mbili na kujikusania pointi 6 huku wakiwa wamefunga magoli manne na kufungwa
goli moja pekee goli lililofungwa kwenye ushindi wao wa goli 3-1 dhidi ya klabu
ya kutoka nchimi Ghana Medeama FC.
Mchezo mwingine katika kundi hili utakuwa kesho wakati timu ya Medeama
itakapokuwa nyumbani kuikaribi9sha klabu ya kutoka Algeria, timu ya Mo Bejaia.
Post a Comment