
KIUNGO mchezaji wa klabu ya Manchester
United, Bastian Schweinsteiger amejumuishwa kwenye kikosi cha watu 25 cha timu
hiyo.
Schweinsteiger
32, bingwa wa kombe la dunia mwaka 2014
na timu ya taifa ya Ujerumani, alikuwa ameambiwa na kocha mkuu wa klabu
hiyo kwamba hayupo tena kwenye mipango yake na hivyo atafute timu nyingine ya
kwenda kuichezea.
Nahodha
huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani, alistaafu mapema mwa wiki iliyopita baada
ya kuifungia timu yake ya taifa magoli 24 kati ya mechi 121 alizocheza nahodha
huyo.
Klabu zote
20 za premia zinatakiwa kuwasilisha majina ya wachezaji 25 ambao kabla ya saa
moja kwa majira ya saa za Africa Mashariki.
Wachezaji
chipukizi kama vile Marcus Rashford, Luke Shaw na Anthony Martial wanaonekana kupewa nafasi kwenye kikosi hicho cha
mabingwa wa zamani wa EPL.
Schweinsteiger,
aliyesajiliwa kwa kandarasi ya miaka
mitatu mwaka jana, alikuwa anafanya mazoezi peke yake na vijana wa miaka 23
tangu Mourinho amekuwa kocha wa klabu hiyo.
Nyota huyo
wa zamani wa klabu ya Bayern Munich amesema yuko tayari kama timu itakuwa inamhitaji,
wakati huo kocha Mourinho amesema Paul Pogba, Marouane Fellaini, Morgan
Schneiderlin, Ander Herrera na Michael Carrick ndio wapo tayari kwenye kikosi
chake
"Tuna
wachezaji watano kwenye sehemu mbili” Mourinho alisema.
Post a Comment