
TIMU
ya
taifa ya Tanzania Taifa Stars, imewasili salama nchini Nigeria tayari kwa
kuivaa timu ya taifa ya Nigeria katika mechi ya kufuzu kuwania tiketi ya kombe
la mataifa ya Africa za mwakani, nchini Gabon.
Kundi la kwanza
liliwasili Abuja jana kwa kutumia shirika la ndege la Ethiopia na kusafiri
kwenda Uyo kwa kutumia jet.
Mwanasheria mkuu wa
shirikisho la mpira nchini Nigeria, Tunde Aderibigbe aliupokea msafara huo na
kusafiri nao mpaka Uyo kabla ya katibu wa NFF kuwapokea huko mji wa Uyo.

Taifa Stars walionekana
wakiwa na amani huku wakiwa kwenye basi lao special walilokuwa wamekodiwa
wakielekea kwenye hotel ya Meridian huku wakitarajiwa kufanya mazoezi ya mwisho
kwenye uwanja watakaochezea hapo kesho.
Taifa Stars watakuwa
wakisaka ushindi wao wa kwanza baada ya kucheza michezo mitano dhidi ya Nigeria
wakiwa wameambulia patupu.

Katika michuano ya kufuzu
kombe la dunia mwaka 1982, timu hizi zilitoka sare ya 1-1 mjini Lagos kabla ya
Tanzania kukubali kichapo cha goli 2-0 hapa Dar es salaam, magoli yaliyofungwa
na John Chidozie na Christian Nwokocha.
Super Eagles waliokuwa
wamepangwa kucheza na Tanzania mwaka 1986, mwaka huu wamepangwa tena kundi moja
huku mchezo wa kwanza ukimalizika jijini Dar es salaam kwa sare tasa,
Timu ya taifa ya
Nigeria, imejipanga kuutumia mchezo huo kama ni mchezo wa kujiandaa na mechi ya
awali ya kusaka tiketi ya kufuzu kombe la dunia la mwaka 2018 dhidi ya timu ya
taifa ya Zambia.
Post a Comment