SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: safari ya yanga bado inaendelea.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
                      Yanga yapata ahueni. Na charle kunji. Baada ya kuishuhudia klabu ya yanga kushindwa kuutumia vyema uwanj...
                      Yanga yapata ahueni.






Na charle kunji.



Baada ya kuishuhudia klabu ya yanga kushindwa kuutumia vyema uwanja wa nyumbani na kukubali kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa mabingwa wa afrika, klabu yaTP MAZEMBE hapo jana katika mchezo ulioisukuma klabu ya yanga nafasi ya mwisho katika msimamo wa kundi A, leo hii klabu ya yanga imeongeza matumaini ya kusonga mbele baada ya wapinzani wao kutoa sare tasa ya bila kufungana.
mpaka filimbi ya mwamuzi inapulizwa katika dakika ya 90, kwenye mchezo wa kombe la shirikisha barania afrika, ambapo wenyeji klabu ya Medeama waliweza kuwakaribisha klabu ya MO bejaia ya nchini Algeria timu hizo zilikuwa hazijafungana na hivyo kuweza kugawana pointi moja kwa moja na kuufanya msimamo wa kundi hilo kusomeka kwa klabu ya TP mazembe kuendelea kuongoza kundi hilo kwa jumla ya pointi 6 huku nafasi ya pili ikishikiliwa na klabu ya nchini algeria MO bejaia kwa jumla ya pointi 4 wakati medeama wakiwa na pointi 1 huku klabu ya yanga ikiwa inaburuza mkia kwa pointi sifuri.
Lakini kwa droo ya mechi ya medeama dhidi ya bejaia inaendelea kuipa matumaini klabu ya yanga kufanya vyema katika kobe la shirikisha barani afrika.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top