
Klabu ya Chelsea imekubali kutoa kitita cha Pauni 32mil kwa
ajili ya kupata kandarasi ya kiungo wa klabu ya Leicester City Ngolo Kante.
Taarifa na skysport.
Leicester City imlimpa Kante kandarasi ya miaka minne kabla
ya mashinfano ya mataifa ya ulaya yaliyofanyika nchini Ufaransa, lakini raia
huyo wa Ufaransa ameiambia klabu hiyo ya kuwa anataka kujiunga na klabuni ya Chelsea.
Knte 25, atakuwa na vipimo vya afya wikiendi hii kabla
hajajiunga na klabu ya Chelsea huko Austria ambako ndio wameweka kambi
wakijiandaa na msimu unaokuja ambapo ataweza kuzungumza hatma ya mkataba wake.
Mkufunzi wa klabu ya Leicester city Claudio Ranieri
amesisitiza ya kuwa angependa kuona Kante akiendelea kuihudumu kabu hiyo, lakini ameelewa ya kuwa Knte kumbe anataka
kuondoka klabuni hapo. Alisema, ‘‘sihitaji kumpoteza Kante, sihitaji kabisa, lakini
ningejua tu kama alikuwa anataka kuondoka”
Kante alikuwa na msimu bora kabisa akiwa na Leicester city na
akiisaidia timu hiyo kutwaa ubingwa wa EPL kwa mara ya kwanza katika historia
ya klabu hiyo huku akicheza mechi 37 pekee. Kane alijiunga na Mbweha wa
jangwani akitokea klabu ya Caen inayoshiriki ligi ya Ufaransa Ligie 1 na kuitwa
kwenye timu ya taifa ya ufaransa na kuweza kucheza chunu ya Deschamps.
Post a Comment