SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Timu ya taifa ya Ukraine Kuwa Chini ya Andriy Shevchenko.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya taifa ya Ukraine imemwajili Andriy Shevchenko kuwa kocha kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo   Mykhaylo Fome...




Timu ya taifa ya Ukraine imemwajili Andriy Shevchenko kuwa kocha kuchukua nafasi ya aliyekuwa kocha wa timu hiyo  Mykhaylo Fomenko ambae amesitishiwa mkataba wake wa miaka miaka minne.
Shevchenko 39, aliyewahi kuzichezea timu za Chelsea pamoja na AC MILAN ya Italia, ameichezea timu ya taifa ya Ukraine mechi 111 na kufunga magoli 48 kabla hajastaafu baada ya mashindano ya EURO yaliyofanyika nchini kwao mwaka 2012, lakini pia akiwa kama nahodha wa timu hiyo, aliweza kuiongoza timu hiyo katika fainali ya kombe la dunia yam waka 2006.
Shevchenko amesaini mkataba wa miaka miwili lakini pia akitarajiwa kuongeza mkataba kama atakuwa na mafanikio katika tiku hiyo. Ukraine itaanza kuisaka tiketi ya kufuzu kombe la dunia la 2018 nyumbani atakapowakaribisha timu ya taifa ya Iceland mwezi September wakiwa kundi moja na Uturuki, Croatia, Finland pamoja na Kosovo.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top