Mchezo huo ulipangwa
kufanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam tarehe 23 Julai, 2016.
Kwa mujibu wa barua
kutoka kwa Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Kenya (FKF), Robert
Muthomi kwenda Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kufuta kwa ziara
hiyo kunatokana na nafasi ambayo Kenya imeipata kwingine.
Timu ya Taifa ya
Vijana ya Kenya imeteuliwa kushiriki michuano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu
la COSAFA inayotarajiwa kuanza Julai 22, 2016 hadi Julai 31, 2016 mara baada ya
Msumbiji kujitoa kwenye mashindano hayo.
Licha ya kwamba mchezo
huo hautakuwapo, ratiba ya Serengeti Boys ambayo inapambana kuwania nafasi ya
kucheza Kombe la Mataifa Afrika hapo mwakani, imebaki vilevile kwa timu kuingia
kambini Jumapili Julai 17, 2016 kwenye Hosteli za TFF zilizoko Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.
Timu
hiyo inayonolewa na Bakari Shime itapiga kambi ya wiki moja katika hosteli
hizo, kabla ya kwenda Madagascar ambako itapiga kambi ya takribani wiki mbili
ikiwa ni ahadi ya Rais wa TFF, Jamal Malinzi ambaye alitoa ofa hiyo baada ya
kuwatoa Shelisheli kwa jumla ya mabao 9-0 katika mechi zake mbili za kimataifa.
Serengeti Boys
inatarajiwa kucheza na Afrika Kusini kati ya Agosti 5, 6 au 7, 2016 huko Afrika
Kusini kabla ya mchezo wa marudiano utakaofanyika saa 9.00 alasiri, Agosti 14,
2016 kwenye Uwanja wa Azam Complex, ulioko Chamazi, Dar es Salaam.
Mshindi wa jumla
katika michezo hiyo, itacheza na timu mshindi kati ya Namibia na
Congo-Brazaville.
Kwingineko,
mchezo wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Tanzania kwa upande wa wanawake
Twiga Stars kucheza dhidi ya timu ya taifa ya wanawake ya Rwanda umefutwa kwa
kile kilichosemekana kutokea kwa mabadiliko ambayo wao hawakuyategemea. Mchezo
huo ulikuwa ni kwaajili ya kuboresha ushirikiano lakini pia ukitarajiwa kuwa
sehemu ya burudani kwa viongozi wan chi za Afrika watakaokuwa na mkutano hapo
nchini Rwanda.
Post a Comment