SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: BAADA YA MANJI KUTANGAZA NIA YAKE YA KUJIUZULU, WANACHAMA WAMSHUKIA MZEE AKILIMALI.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Picha na salehe jembe. SAKATA la mwenyekiti wa klabu ya Yanga, limechukua sura mpya leo baada ya wanachama wa klabu hiyo kukubaliana...
Picha na salehe jembe.

SAKATA la mwenyekiti wa klabu ya Yanga, limechukua sura mpya leo baada ya wanachama wa klabu hiyo kukubaliana kwamba moja ya wazee wa klabu hiyo, Mzee Akilimali, asimamishwe kwa muda, kwa  kile kinachodaiwa kwamba ni moja ya watu waliopelekea Manji aachie nafasi hiyo ya uwenyekiti pamoja na kusitisha zoezi la kuikidosha klabu hiyo kwa miaka kumi.

Hapo jana Yusuf Manji alitangaza nia yake ya kutaka kujiuzulu kuwa mwenyekiti wa klabu hiyo ya jangwani na kusema kuwa kuna watu wanaofanya yeye afikie maamuzi hayo kwani matusi yamezidi sana.


Aidha, baada ya wanachama kukutana leo makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mtaa wa jangwani, wengi wao walikuwa wanataka mzee Akilimali asimamishwe kwa muda kwani ndiye cha cha matatizo yote ya hapo klabuni.

Wakati alipopigiwa simu na mtandao wa www.salehejembe.blogspot.com, mzee Akilimali alisema kuwa amekwenda kumaliza tofauti na hivyo wamsubiri atarudi.

Hata hivyo, baada ya kuonekana kwenye makao makuu yay a klabu hiyo, wanachama wengi wa klabu hiyo waliokuwa wanaongea kwa jazba, walitaka viongozi wa klabu hiyo wamsimamishe mzee huyo kwa muda kwani amekuwa ni kikwazo klabuni hapo.

Hata hivyo, kutokana na taarifa za ndani za www.charleskunji.blogspot.com, imeripotiwa kwamba kikao cha viongozi wa klabu hiyo ya jangwani, wamekubaliana kumsimamisha mzee Akilimali kwa muda, ili kupisha mambo mengine yaendelee ndani ya klabu, kwani kwa uwepo wake, ni kama kikwazo kwa baadhi ya vitu kutokea.

Suala la Manji la kujiuzulu bado halijabatilishwa na mwenyekiti huyo, na uongozi wa klabu ya Yanga, wanasubiri barua rasmi ya kiongozi huyo kama kweli anataka kujiuzulu, ingawaje bado kuna taarifa ambazo zimekuwa zikivumishwa ya kwamba Manji atarejea klabuni hapo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top