
Mcheza tenisi nambari
moja nchini Wingereza Johana Konta ametinga hatua ya robo fainali ya Rogers Cup
yanayoendelea huko nchini Canada baada ya kumshinda kwa jumla ya set 6-3 6-2
Mmarekani Varvara Lepchenko.
Konta mwenye umri wa miaka
25 atachuana na Kristina Kucova mwenye miaka 26 katika hatua ya nusu fainali
baada ya raia huyo wa Slovakia kumfunga mwenyeji wa mshindano hayo Eugenue
Bouchard kwa jumla ya set 3-6 6-4
6-3.
Mcheza tenisi namba 14 duniani Venus Williams amepoteza mchezo wke dhidi
ya Mmarekani mwenzake Madison Keys. Williams 36, aliyepigwa pia na Johana Konta
katika fainali za Stanfford Classic, alikubali kichapo cha set 6-1 6-7 (2-7)
6-3.
Na kwa upande wa wanaume, mcheza tenisi namba 1 Novak Djokovic hakuwa na
wakati mgumu kuelekea robo fainali baada ya kumfunga Radek
Stepanek raia wa jamhuri ya Cheki kwa set 6-2 6-4.
Djokovic, raia wa Serbia sasa atakutana na
mcheza tenisi namba 8 Tomas Berdych.
Kipigo cha mwaka huu cha Wembleydon dhidi ya Andy Murray alikuwa na
mteremko baada ya kumfunga raia wa Marekani Jared Donaldson 19 kwa set 6-2 6-3.
Post a Comment