SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Bastian Schweinsteiger Aruhusiwa Kutafuta Timu Nyingine.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Bastian Schweinsteiger, raia wa Ujwerumani aliyeiongoza timu ya taifa ya Ujerumani kutwaa kombe la dunia mwaka 2014, nafasi yake ka...

Bastian Schweinsteiger


Bastian Schweinsteiger, raia wa Ujwerumani aliyeiongoza timu ya taifa ya Ujerumani kutwaa kombe la dunia mwaka 2014, nafasi yake katika klabu ya Manchester United imekuwa ni ya mashaka tangu ujio wa kocha mpya Jose Morinho.

Morinho amekwishafanya usajili wa wachezaji watatu na anakaribia kukamilisha dili na kiungo wa timu ya taifa ya Ufaransa na klabu ya Juventus Paul Pogba,

Bastian Schweinsteiger 31, anaonekana ni moja ya list ya wale wachezaji 9 watakaotemwa na kocha huyo raia wa Ureno. Schweinsteiger ambae ametangaza kustaafu soka la kimataifa, ameonekana akifanya mazoezi akiwa peke yake wakati kikosi kamili cha United kikifanya nazoezi ya jumla kwa siku ya kwanza.

Washambuliaji Adnan Januzaj, Will Keane na James Wilson kiungo Andreas Pereira na mabeki Cameron Borthwick-Jackson, Tim Fosu-Mensah, Tyler Blackett na Paddy McNair wameripotiwa kutafuta timu za kwenda kwa mkopo au kusajiliwa moja kwa moja. Pamoja wachezaji wa kikosi cha kwanza kutokuwepo kwenye tour ya nchini China, Schweinsteiger kutojumuika na wenzake katika mazoezi ya siku ya jana, kunathibitisha rasmi ya kuwa huenda akaondoka klabuni hapo.

United inaripotiwa ililipa kiasi cha pauni mil14.4 kupata kandarasi ya Schweinsteiger kutoka klabu ya Bayern Munich miezi 12 iliyopita lakini usajili huo haukufikia malengo na mkufunzi huyo.

Majeraha yalimfanya Schweinsteiger kucheza mechi 31 pekee huku akikosa fainali saba ikiwemo ile ya FA United walipoifunga Crystal Palace kwa ushindi wa goli 2-1. Alipata jeraha la goti katika 
mashindano ya EURO ya mwaka huu alipoamua kustaafu kucheza timu ya taifa huku akifunga goli 1 mechi walipocheza na timu ya taifa ya Ukraine.

Kocha wa sasa wa timu ya Manchester United Jose Morinho anaonekana kutopendelea kutumia vijana haswa wale waliokuwa wanakuzwa na kocha wa zamani wa klabu hiyo Louis Van Gaal ambae ameshindwa kuipa mafanikio klabu hiyo.




About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top