SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Johanna Konta asonga mbele Rogers Cup
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mcheza Tenisi nambari moja kwa Uingereza Johanna Konta ameifikia hatua ya tatu ya Rogers Cup kwa kumchapa Mmarekani Vania King. Mwana d...
Johanna Konta
Mcheza Tenisi nambari moja kwa Uingereza Johanna Konta ameifikia hatua ya tatu ya Rogers Cup kwa kumchapa Mmarekani Vania King.
Mwana dada huyo amefikia hatua hiyo kwa ushindi wa 7-5 6-1 dhidi ya King.
Johanna Konta ambaye katika uchezaji Duniani yuko kwenye nafasi ya 14, katika hatua inayofuata atakutana na Mmarekani Varvara Lepchenko
Wakati mashindano ya Rogers Cup yakiendelea, idadi ya wachezaji wa tenesi kuendelea kujiengua katika mashindano ya Olympic Yazidi kuongezeka baada ya mchezaji Belinda Bencic anayeshikila namab 16 kwa viwango vya tenisi duniani kujitoa katika mashindano ya Olympic yatakayoanza tarehe 5 ya mwezi ujao.

Belinda Bencic

Bencic 19, raia wa Uswis alilazimika kujitoa katika raund ya pili ya Wembleydon baada ya kupata maumivu ya kifundo cha mkono, ametoa taarifa kupitia mitandao yake ya kijamii ya kuwa hatoshiriki Olympic na badala yake muda wote huo atakuwa akijianda na mashindano ya US Open ambayo yanatarajiwa kuanza tarehe 29 ya mwezi ujao, siku moja baada ya Olympic kufikia kikomo chake.
Hivyo list ya wachezaji wa tenisi ambao hawatoshiriki Olympic ni Maria Sharapova ambae yeye alifungiwa kwa muda baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kusisimua misuli, Lakini pia Victoria Azarenka nae hatashiriki kwa sababu ya kuwa na ujauzito pamoja na Simona Halep pamoja na Karolina Piscova.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top