
Kocha wa klabu
ya Liverpool, Jurgen Klopp, ametanabaisha sababu za kumrudisha nyumbani beki
wake Mamadou Sakho badala ya kubaki naye katika kambi waliyoweka nchini
Marekani.
Klopp amesema kwamba Sakho, ambaye hivi karibuni
aliondolewa adhabu yake ya kufungiwa kutokana na tuhuma za matumizi ya madawa
ya kusisimua misuli, alivunja sheria za klabu hiyo mara tatu na sasa ana
hatihati ya kutemwa ikiwa kocha huyo atachukua maamuzi mazito zaidi.
“Ilikuwa ni almanusura achelewe ndege ambayo ilikuwa
ikibeba timu kutoka Liverpool kwenda San Francisco, alikosa kufanya mazoezi na
timu na pia alichelewa kujumuika na wenzake kupata chakula,” alisema Klopp
Natakiwa kutengeneza kikosi hapa na tunapaswa kuanzia
hapa. Nilidhani pengine kulikuwa na ulazima wa yeye kurudi Liverpool sasa.
“Tuna sheria zetu hapa ambazo tunapaswa kuziheshimu, kama
kuna mtu naona hafanyi hivyo, lazima nichukue hatua.
Baada ya siku nane au kumi tunaweza kuzungumza juu ya
hilo. Hatukuwa na mazungumzo yoyote lakini nilimweleza, huwezi kujibana wakati
anayeongea ni mtu mmoja.”
Alipoulizwa kama Sakho atapigwa faini, Klopp alisema
angependa kuona adhabu mbadala ikichukuliwa kwasababu asingependa kukurupuka
kutoa maamuzi.
“Kumpiga faini? Unaweza kuuliza, na naweza kulielezea
hilo kwa undani zaidi,” alisema Mjerumani huyo.
“Sipendezewi na adhabu za kutoza wachezaji fedha, kiukweli
hii haitokei mara kwa mara kwenye maisha yangu, naweza kumpiga faini mtu yoyote
lakini sipendi kwasababu nataka tuwe na nidhamu, tujifunze pamoja na kufanya
yaliyo sahihi.
“Sehemu zote ambazo nimepita, huwa sipendi utaratibu huo,
ni jambo la kufurahisha, lakini unapompiga mtu faini halafu akarudia kosa
utakuwa umemsiadia nini, mara nyingi faini huwa haisaidii.
“Si kana kwamba wanajali sana pesa, ila unakuta wakati
anatoa pesa anakuwa anaumia lakini baada ya muda anasahau. Hivyo, nataka
wachezaji wote wafuate yale yote ambayo yapo kwenye utaratibu wetu.”

Na katika hatua nyingine,
klabu ya Liverpool wameweza kukubali kichapo cha goli 1-0 dhidi ya timu ya
Chelsea katika mwendelezo wa michezo ya kirafiki inayoendelea huko nchini
Marekani, China pamoja na Austria, zikiwa mechi mahsusi kwa ajili ya kujiandaa
ni msimu mpya unaoanza mwezi ujao.
Post a Comment