SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Guardiola Na Mbio Za Kuandaa Timu Bora.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kocha mpya wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola, ameandikisha ushindi wake wa kwanza tangu atue Manchester City baada ya kuwaongoza...
Kocha mpya wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola, ameandikisha ushindi wake wa kwanza tangu atue Manchester City baada ya kuwaongoza mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu ya Uingereza kuwalaza Borussia Dortmund katika kinyang'anyiro cha kutafuta mabingwa wa vilabu vya kimataifa huko nchini China.
Kipa chipukizi wa Man City Angus Gunn, 20, aliokoa mkwaju wa penalti wa Mikel Morino na kuwahakikishia vijana wa Pep ushindi wa mabao 6-5.
Mechi hiyo iliyochezwa katika uwanja wa Longgang ulioko Shenzhen ilikuwa imeishia sare ya 1-1 katika muda wa kawaida.
Sergio Aguero alikuwa ameiweka Man City kifua mbele mapema katika mechi hiyo lakini mshambuliaji chipukizi wa Dortmund Christian Pulisic, mwenye umri wa miaka 17, akawasawazishia wajerumani hao katika muda wa majeruhi.
Hii ndio ilikuwa mechi yao ya pili baada ya ile ya kwanza kwa Man City kupoteza mbele ya Bayern Munich kwa goli 1-0, baada ya mechi iliyokuwa imepangwa awali dhidi ya vibonde wao wa jadi kutoka Uingereza Manchester United kuahirishwa kufuatia mvua kubwa iliyonyesha mjini Beijing.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top