
Pep Guardiola amewasimamisha baadhi ya wachezaji kwenye kikosi
cha Manchester City kufanya mazoezi kufuatia kuongezeka uzito kupita kiasi.
Awali, iliripotiwa
kuwa Yaya Toure na Samir Nasri walikuwa wahusika wakuu katika suala hili ili
kuwafanya warudi katika hali yao ya kawaida.
Japokuwa
hakutaja mtu yeyote, beki wa kushoto wa klabu hiyo Gael Clichy ametanabaisha
kwamba kuna baadhi ya wachezaji ambao kocha aliwaengua mpaka pale timu
ilipokwenda nchini China.
Ndani ya kikosi
cha Manchester City, mambo yanaonekana kuwa tofauti sana ukilinganisha na
awali, Hayo yote yametanabaishwa na beki wa miamba hao Clichy.
“Ndani ya
uwanja, nje ya uwanja, kila kitu kinachukuliwa kwa umakini,” Clichy aliwaambia
waandishi. Kwa mfano, mara nyingi unasikia mameneja wakisema kuwa na afya bora
ni muhimu. Sasa kwake yeye, kama uzito wako ni mkubwa sana, basi haufanyi
mazoezi na timu.
“Hiko ndicho
kitu cha kwanza na nimekuwa nikisikia mara nyingi sana lakini kwangu mimi ni
mara ya kwanza kuona meneja akifanya hivyo. Hivyo tuna wachezaji wachache ambao
bado hawafanyi mazoezi na timu, ni suala la kufurahisha kidogo, lakini sisi
tunacheza soka na ni ndio kazi yetu na pia tunapaswa kuwajibika kwa kile tunachokifanya
uwanjani.”
Bila shaka
unaweza kuwa na ubora lakini unapaswa kujua kwamba kama uzito wako ni kilo 60
halafu uko kwenye kilo 70, basi hauwezi kucheza mpira kwa sababu utapata
majeraha na kuiweka timu yako katika wakati mgumu.”
Guardiola pia
amegusia juu ya mpango mpya wa chakula kwa wachezaji wake, hasa piza, chakula
ambacho kimekuwa kikitumiwa na wachezaji wa timu yake baada ya mechi katika
miaka ya hivi karibuni na vitu vingine sasa vimepigwa marufuku.
“Amepiga
marufuku baadhi ya juisi na bila shaka piza na vyakula vyote vizito-vizito
haviruhusiwi,” Clichy aliongeza. “Ni kitu cha kawaida lakini watu wengine
wanadhani kwamba, ni kawaida mno, ingetakiwa kuwa hivi, lakini kiukweli sio
kila kitu kunakuwa kama hivi na najua kwasababu nimekuwa nikicheza soka kwa
muda mrefu sasa. Inasisimua kwa kweli.”
Wachezaji wengi
ambao walikuwa kwenye timu zao za taifa, wameungana na wenzao katika kikosi cha
Manchester City nchini China, lakini Clichy anasema kwamba wapo pale kwa
geresha lakini watakuwa fiti zaidi watakaporejea England.
Post a Comment