![]() |
picha na boiplus. |
LIGI kuu Tanzania bara, VPL, imeendelea leo ambapo katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam wenyeji African Lyon waliwakaribisha timu ya Ndanda FC ya mjini Mtwara ambapo wenyeji African Lyon wameibuka na ushindi wa goli 1-0.
Goli pekee la Lyon liliwekwa kimiani na kiungo, William Otong dakika ya 75 baada ya kuunganisha mpira uliopigwa na Omary Salum.
Baada ya takribani wiki nane, timu ya Majimaji FC chini ya Kalimangonga Ongala wameweza kupata ushindi wa kwanza baada ya kuifunga Mbao FC goli 1-0 wakati katika uwanja wa Manungu mjini Tuliani, Mtibwa Sugar wamelazimishwa sare tasa na timu ya JKT ruvu.
Ligi hiyo itaendelea tena katikati ya wiki ijayo ambapo vinara wa ligi hiyo, Simba watakuwa wageni wa Mbeya City katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine.
Post a Comment