SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: YANGA KUFANYA MKUTANO WA DHARURA.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KULINGANA na taarifa zilizotufikia hivi punde, ni kwamba uongozi wa klabu ya Yanga umeamua kuitisha mkutano wa dharura ambao utafanyi...


KULINGANA na taarifa zilizotufikia hivi punde, ni kwamba uongozi wa klabu ya Yanga umeamua kuitisha mkutano wa dharura ambao utafanyika October 23 ya mwaka huu.

Mkutano huo ambao utafanyika siku ya jumapili, utatangazwa ni wapi utakapofanyika kama kila kitu kitakwenda sawasawa.

"Ukumbi utatangazwa, lakini kama uongozi, tumeamua kuitisha mkutano huo" Alisema.

Ajenda za mkutano huo hazijawekwa wazi japo huenda likawa ni lile sakata la klabu kufanya mabadiliko ya kutaka kukodisha timu hiyo kwa mwenyekiti wa klabu hiyo, Bwana Manji.

Ikumbukwe ya kuwa BMT waliijia juu klabu ya Yanga juu ya maamuzi yao ya kutaka kuikodisha timu ya kuwa ni lazma kanuni na sheria ni lazima zifuatwe.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top