
ALIYEKUWA boss wa zamani wa timu ya
Birmingham City, Steve Bruce ameendelea na mazungumzo na mabosi wa timu ya Aston
Villa na kuonyesha dalili za kuwa huenda akatangazwa kuwa kocha mpya wa Aston
Villa baada ya kumtimua Roberto di Matteo siku ya jumatatu huku akiiacha klabu
ikiwa nafasi ya 19 kwenye championship.
Bruce, 55,
alikuwa hana timu yeyote kwa muda sasa japo alikuwa na interview ya kuitaka nafasi
ya kuwa kocha wa timu ya England ambapo pia mipango haikumwendea sawa.
Msaidizi
wa Di Matteo Steve Clarke ataendelea kubakia klabuni kama msaidizi na
ataiongoza timu hiyo itakapokuwa na mchezo kwenye uwanja wa nyumbnai dhidi ya
timu ya Wolverhampton Wanderers, 15 October.
Mchezaji
wa zamani wa timu ya Birmingham, Robbie Savage, ambaye aliwahi kufundishwa na
Bruce, amemuelezea Bruce ya kuwa ni mtu
sahihi wa kuja kuifundisha klabu ya Aston Villa.
"Steve
Bruce amekuwa na mazungumzo ya kina Zaidi ya mara tatu ndani ya masaa 48 na
wakuu wa Aston Villa, ingawaje bado ni kama wanauficha ukweli. Kililipoti kituo
kimoja cha redio cha nchini England.
Hata
hivyo, mazungumzo Zaidi na mmiliki wa klbau hiyo, bwana Tony Xia bado
hayajaanza lakini wachambuzi wa masuala ya soka nchini huko wanaamini Bruce ni
mtu sahihi wa kuiongoza klabu hiyo na hata kuirejesha ligi kuu.
Di Matheo
amecheza mechi nane na hajapata ushindi hata mmoja atngu apewe timu hiyo.
Post a Comment