
MCHEZAJI wa zamani wa timu Arsenal, Alexander
Hleb anaamini kwamba kikosi cha sasa cha Arsene Wenger kina uwezo wa kubeba
mataji matatu kwa mpigo msimu huu
Arsenal
wamekuwa na matokeo mazuri katika michezo ya hivi karibuni, wakiwa na alama
mbili nyuma ya vinara wa EPL, klabu ya Manchester City vilevile wakiwa
wamejikusanyia alama nne katika michezo miwili kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Hleb
ambaye wakati yupo Arsenal hakuwahi kushinda taji lolote anaona ubora wa sasa
wa Arsenal ni wa kuchukua mataji matatu msimu huu.
“Naamini
Arsenal watashinda mataji matatu msimu hu, ubingwa wa Premier League, Kombe la
FA na Ligi ya Mabingwa pia,”Hleb amesema. ” Naiona Arsenal yenye uwezo na ari
ya kupambana na kwa hakika nitaisapoti.”
“Mara
nyingi Wenger huwa ana matarajio makubwa. Ameweza kuwabakisha wachezaji wake
muhimu wote kwa sasa na wanacheza mpira mkubwa mno. Kila mpinzani wao lazima
aingiwe na hofu!”
Post a Comment