FAINALI EURO 2012 YARUDISHWA HATUA YA MTOANO

Na Charles Kunji
Michuano ya EURO2016
inaendelea leo huko nchini ufaransa kwa kuzikutanisha timu ya Italy kuwavaa
SPAIN ikiwa ni marudio ya mechi ya fainali ya EURO2012 iliyofanyika huko nchini
Poland pamoja na Ukeaine.
Katika fainali hiyo, Italy
waliweza kukubali kichapo cha magoli manne kwa nunge na hivyo kuwatawaza
mabingwa Hispania wakiwa wamechukua kombe hilo mwaka 2008 lakini pia kuchukua
tena kombe la dunia mwaka 2010 lililofanyika kwenye ardhi ya afrika kwa mara ya
kwanza.
Katika ushindi wa magoli
manne walikuwa ni akina Silva, Alba,Torres pamoja
na Mata ndio walioinogesha fainali hiyo huku
wakipeleka msiba mzito nchini Italy.
Leo June 27 wanakutana tena katika mashindano hayahaya lakini
ikiwa ni hatua ya mtoano. Swali la timu ya Italy kulipiza kisasi litajibiwa
baada ya filimbi yamwisho ya mwamuzi wa mchezo huo.
Mechi nyingine ya siku ya leo itawakutanisha England wakiwakabili
Iceland huku kukiwa na habari zisizo njema sana kwamba yule mnyama anayetabir
mechi mbalimbali, akitabiri ya kuwa England watapoteza mchezo huo. Macho na
masikio ya wapenda soka yatakuwa yakisubiri kwa hamu matokeo ya mechi hii.
Lakini katika michezo ya siku ya jana, Wenyeji ufaransa
walitokea nyuma na kuweza kushinda mechi yao dhidi ya Ireland ushindi wa magoli
mawili kwa moja yote yakiwekwa wavuni na mshambuliaji wa kimataifa Antonio
Greezeman anayekipika katika klabu ya Athletical Madrid ya nchini Hispania.
Mabingwa wa kombe la dunia mwaka 2014 waliweza kuwabugiza
Slovkia mabao matatu kwa sifuri magoli yaliyowekwa kimwani na Jelome Buateng,
Mario Gomez pamoja na Julian Draxler huku Mesuit Ozil akikosa mkwaju wa penaty.
Mechi ya mwisho kwa siku ya jana iliweza kushuhudia ubelgiji
wakiibuga kwa ushindi mnono wa magoli manne kwa sifuri magoli yaliyofungwa na Toby
Alderweireld, Yannick Ferreira-Carrasco pamoja na Eden Hazard.
Post a Comment