SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Wengine wamfuata messi
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
                        Baada ya LIONEL MESSI, wengine wakafuta. Na Charles Kunji . Hii ni siku mbaya kwa soka la Argentina...


                        Baada ya LIONEL MESSI, wengine wakafuta.







Na Charles Kunji.
Hii ni siku mbaya kwa soka la Argentina, baada ya kushindwa kutwaa taji la Copa America kwenye mchezo wa fainali dhidi ya Chile, uliofanyika asubuhi ya leo, wachezaji wa Argentina mmoja baada ya mwingine wamekuwa wakitangaza kustaafu kuichezea timu yao ya taifa.
Mchezaji wa kwanza kutangaza kustaafu kuitumikia timu hiyo alikuwa Leo Messi ambaye alitangaza uamuzi huo muda mfupi baada ya mchezo dhidi ya Chile kumalizika.
Maamuzi hayo yaemukuja punde baada ya Lionel Messi kukosa mkwaju wa penalty uliopelekea timu yake ya taifa kulikosa kombe la Copa Amerika kwa mara ya pili mfululizo mikononi mwa Argentina.
Muda mfupi baadaye striker wa Manchester City Sergio Aguero na mlinzi wa kati wa FC Barcelona Javier Mascherano nao pia walitanga kuachana na timu katika soka la kimataifa.
Kama vile haitoshi, ripoti kutoka Amerika ya Kusini zinadai kuwa, Angel Di Maria, Ezequiel Lavezzi, Gonzalo Higuain na Lucas Biglia nao pia wameamua kutundika daruga kuitumikia Argentina.
Laikini kocha wa timu hiyo Tata Martino hajachukua uamuazi wa kuikacha timu hiyo na labda tumpe muda ni linin aye atatoa hatima yake ama ataendelea kuitumikia timu hiyo au laaah.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top