SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: hispania yatupwa nje ya mashindano.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
         Italy kufuta uteja dhidi ya hispania. Na Charles Kunji Hakika ule msemo usemao, mtu hawezi kufa mara mbili umeweza ku...
         Italy kufuta uteja dhidi ya hispania.







Na Charles Kunji




Hakika ule msemo usemao, mtu hawezi kufa mara mbili umeweza kujidhihirisha katika dimba la stade de france baada ya kushuhudiwa mabingwa watetezi wa kombe la EURO kufungwa 2-0 dhidi ya timu ya taifa ya Italy.
Katika mchezo uliozikutanisha timu hizi kawenye kombe la EURO 2012, katika hatua ya fainali, Italy iliweza kukubali kichapo cha magoli 4-0 magoli yaliyopachikwa kimiyani na Alba, Torres, Silva pamija na Mata na kuifanya uhispania kunyakua kombe hilo.
Katika mashindano ya EURO2016, Hispania na Italy wameweza kukutana katika hatua ya 16 bora yaani hatua ya mtoano na kushuhudia timu ya taifa ya Italy kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 magoli yaliyowekwa nyavuni na Girgio Chiellin pamoja na pamoja na Graziano Pelle mshambuliaji wa kimataifa anayekipiga katika klabu ya Southampton ya nchini wingereza.
Timu ya taifa ya Hispania iliyosheheni majina makubwa kama vile David Silva, Busqet, Iniesta, David Degea, Norito pamoja na wengineo wengi, ilikuwa inapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri n ahata kuchukua kombe hilo lakini mambo yamekuwa tofauti kwa timu ya Italy kupindua matokeo na kuweza kufuta uteja kwa uhispania.

Katika mchezo unaoendelea, wingereza bado iko nyuma kwa goli 2-1 dhidi ya timu ya Iceland. Magoli ya Iceland yametiwa kimyani na Ragnar Sigurdsson na Kolbeinn Sigthorsson huku goli la wingereza likifungwa na nahodha Wayne Rooney kwa mkwaju wa penalty katika dakika ya 4 ya mchezo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top