SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: SAMATTA AZIDI KUCHANJA MBUGA ULAYA, AWEKA REKODI NYINGINE.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
HII ni habari njema kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania baada ya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, na mshambuliaji wa klabu ...



HII ni habari njema kwa mashabiki wa soka nchini Tanzania baada ya nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, na mshambuliaji wa klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Ally Samatta kuendelea kufanya vyema kwenye soka la kulipwa huko barani ulaya.

Muda mchache uliopita Genk walikuwa na mchezo wa marudiano wa Europa League na kufanikiwa kusonga mbele baada ya kulazimishwa sare na mahasimu wenzao toka nchini humo klabu ya Gent.

Mchezo wa awali ulimalizika kwa Genk kushinda jumla ya mabao 5-2 huku Samatta akipachika wavuni magoli mawili na baada ya sare ya leo, Genk sasa wanafuzu hatua ya robo fainali kwa jumla ya mabao 6-3.

Licha ya kucheza dakika zote 90, Samatta hakufanikiwa kuzifumania nyavu ma hivyo kushindwa kuendeleza moto wake wa kufumga mechi nne mfululizo.

Samatta anakuwa mchezaji wa kwanza toka Tanzania kufika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ulaya na hivyo kusubiri droo itakayopangwa hapo baadae.

Hata hivyo Samatta mwenyewe alipokuwa akifanya mahojiano na mtangazaji wa kipindi cha sports extra cha clouds, bwana Shaffih Dauda, Samatta alionyesha waziwazi ya kuwa anatamani kupangwa na klabu ya Manchester United kwani anahisi ndoto zake zitakuwa zimetimia.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top