SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: PLUIJM AULA SINGINDA UNITED, ASAINI KANDARASI YA MIAKA MIWILI.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  BAADA ya kusambaa kwa picha kwenye mitandao ya kijamii ya aliyekuwa kocha wa zamani wa Yanga, Hans Van Pluijm, juu ya kujiunga na S...
 


BAADA ya kusambaa kwa picha kwenye mitandao ya kijamii ya aliyekuwa kocha wa zamani wa Yanga, Hans Van Pluijm, juu ya kujiunga na Singida United, sasa ni rasmi kocha huyo atakuwa mkufunzi wa klabu hiyo.

Pluijm ametia kandarasi ya miaka miwili na hivyo anatarajia kuleta mapinduzi makubwa kwenye soka la bongo kwa uzoefu ambao tayari alishakuwa nao.

Uongozi wa Singida United umetoa taarifa rasmi kwa umma kuthibitisha kumsainisha kocha huyo mkataba wa miaka miwili kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.


Hans alikuwa kama mkurugenzi wa benchi la ufundi la Yanga ambao waliamua kusitisha mkataba wake baada ya kuona cheo hicho hakikuwa na maana sana kwa sasa.


Hans ametambulishwa na kinda mwingine Tafadwaza Katinyu kutoka Zimbabwe kama mchezaji na kuja kuongeza nguvu ya kiungo ya klabu ya Singida United ambao ni wageni wa ligi kuu ya VPL.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top