SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: VPL INAREJEA TENA WIKIENDI HII.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
BAADA ya mapumziko ya takribani ya wiki tatu kupisha michuano mbalimbali ya kimataifa kwa ngazi ya timu ya taifa na klabu, kadhalika m...

BAADA ya mapumziko ya takribani ya wiki tatu kupisha michuano mbalimbali ya kimataifa kwa ngazi ya timu ya taifa na klabu, kadhalika michuano ya Kombe la Azam Sports Federation Cup, Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inarejea tena leo Jumamosi April 1, 2017 kwa michezo miwili.
Mechi ya kwanza itawakutanisha mabingwa watetezi wa ligi hiyo, timu ya Yanga watakaokuwa wakichuana vikali na matajiri wa jiji la DSM, timu ya Azam FC kwenye dimba la taifa majira ya saa kumi za jioni.
Kadhalika, katika uwanja wa kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya, Mbeya city watakuwa wenyeji wa Ruvu shooting yenye makazi yao Mlandizi mjini Pwani.
Mechi za ligi hiyo ambazo huoneshwa mubashara na Kituo cha Televisheni cha Azam ambacho ni mdhamini mwenza wa VPL, itaendelea kesho Jumapili April 2, 2017 ambako Kagera Sugar inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba mkoani Kagera. Mchezo huo utakuwa saa 10:00 jioni.
Mchezo mwingine utazikutanisha timu za African Lyon ya Dar es Salaam dhidi Stand United ya Shinyanga utakaofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Mchezo huu, utaanza saa 8:00 mchana kwa kuwa kanuni zinaridhia.
Mtibwa Sugar ya Morogoro watakuwa wageni wa Tanzania Prisons ya Mbeya kwenye Uwanja wa Sokoine jijini humo wakati Mwadui FC, kwa upende wake watawaalika JKT Ruvu ya Pwani kwenye Uwanja wa Mwadui huko Shinyanga huku Majimaji wakiwa ni wenyeji wa Toto Africans kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top