SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: SADIO MANE NA WENZAKE WAIADHIBU EVERTON, WAPAA HADI NAFASI YA TATU.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
LIGI kuu nchini England imerejea tena kwa kasi ambapo leo kwenye mchezo wa awali ulikuwa ukiwakutanisha mahasimu wa ligi hiyo, klabu y...




LIGI kuu nchini England imerejea tena kwa kasi ambapo leo kwenye mchezo wa awali ulikuwa ukiwakutanisha mahasimu wa ligi hiyo, klabu ya Liverpool waliokuwa na kibarua cha kuwakabiri Everton kwenye uwanja wa nyumbani wa Liverpool, Anfield.

Dakika 90 za mtanange huo zimemalizika kwa Liverpool kuibuka na ushindi wa magoli 3-1 na hivyo kujikita kwenye nafasi za juu za msimamo wa ligi hiyo mpaka nafasi ya tatu. Kwa jumla ya pointi 59.
Alikuwa na Sadio Mane aliyeanzisha hazina ya mabao ya Liverpool mnamo dakika ya 8 akigongea pasi mujarabu na Roberto Firmino.

Hata hivyo goli la Mane halikudumu kwani dakika ya 28 beki wa Everton, Matthew Pennington alipachika bao na hivyo kufanya ubao ukisomeka 1-1 na mpaka dakika 45 zinamalizika, Coutinho akaifungia Liverpool bao la pili na hivyo kufanya timu hizo kwenda mapumziko kwa liver kuongoza kwa 2-1.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo kila timu ilikuwa inatafuta nafasi ya kufunga goliili kuibuka na ushindi wa pointi tatu.

Dakika ya 60, Divock Origi akapachika bao la 3 kwa Liverpool na goli la ushindi kwenye mchezo huo uliomalizika muda si mrefu.


Kwa matokeo hayo Liverpooll wanajikita kwenye nafasi ya 3 wakiwa na pointi 59 nyuma ya vinara wa ligi hiyo klabu ya Chelsea walio na pointi 69.

About Author

Advertisement

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Post a Comment

 
Top