SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: AHMAD AMBWAGA HAYATOU KWENYE NAFASI YA URAISI WA CAF.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
RAIS  wa chama cha soka nchini Madagascar Ahmad Ahmad ameushtua ulimwengu wa soka baada ya kumbwaga Issa Hayatou ambaye alikuwa rais wa m...
New Caf president Ahmad is held aloft
RAIS wa chama cha soka nchini Madagascar Ahmad Ahmad ameushtua ulimwengu wa soka baada ya kumbwaga Issa Hayatou ambaye alikuwa rais wa muda mrefu wa shirikisho la soka Afrika na kushinda urais wa Caf leo March 16, 2017.
Ahmad Ahmad amechaguliwa kwa jumla ya kura 30 huku akimbwaga mbali mpinzani wake Issa Hayatou kwa kura 20.
Kwa matokeo hayo, sasa mtawala wa karibu miongo mitatu Issa Hayatou sasa atakuwa amemaliza muda wake wa utawala na kumpisha Ahmad Ahmad.
Mipango na mbinu kabla ya uchaguzi zimepelea kuwashangaza wengi baada ya kushuhudia kambi ya Hayatou ikidondoshwa.
Hayatou mwenye miaka 70 sasa, alikuwa rais wa CAF tangu mwaka 1988 wakati huo ambao Lionel Messi alikuwa na miezi tisa tu tangu azaliwe wakati mtawala huyo mzaliwa wa Cameroon alipotangazwa kusimamia soka la bara la Afrika.
Alianza kutawala tangu March 10, 1988 alikuwa anaifukuzia rekodi ya kuendelea kusalia madarakani kwa awamu ya nane mfululizo.
Uchaguzi ulifanyika leo baada ya mkutano mkuu wa 39 huko mjini Addis Ababa.
Ahmad anakuwa rais wa saba wa CAF kwenye historia ya shirikisho hilo lenye miaka 60 hadi sasa tangu kuanzishwa kwake.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top