SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Akina KANAVARO Sio kizazi cha Kesho
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wakati timu ya taifa ya Wales ikiwashangaza mashabiki wa mpira wa miguu kwa kufanya vyema katika mashindano yaanyoendelea nchini Ufaransa...
Wakati timu ya taifa ya Wales ikiwashangaza mashabiki wa mpira wa miguu kwa kufanya vyema katika mashindano yaanyoendelea nchini Ufaransa, licha ya kutolewa katika hatua ya nusu fainali dhidi ya timu ya taifa ya Ureno, iliwalazimu Wales kusubiri hadi miaka 58 ya kuwa na kizazi bora kabisa cha wachezaji waloiinyesha ubora wa hali ya juu.
Kufuzu katika michuano mikubwa kama hii, kwa mara ya mwisha taifa hili dogo likiwa sehemu ya nchi ya Uingereza, ilikuwa ni mwaka 1958 na tangu hapo hawajafanya vyema mpaka kizazi cha akina Gareth Bale pamoja na Aron Ramsey walioweza kuiongoza timu ya Wales kufika hapa ilipofika. Pengine unaweza usitambue umuhimu wa timu ya vijana, Cape Verde lakini unapoona Mataifa kama Cape Verde, Mouritius wakifanya vyema walikubali kusubiri hadi hapo watakapokuwa na timu bora ya vijana na kuwakuza ambao sasa wanifanya Cape verde waingie tano bora ya Mataifa ya Africa katika viwango vya FIFA.
Tanzania pamoja na kuitwa majina mengi yakiwemo, kichwa cha mwendawazimu sababu ikiwa ni kutokufanya vyema kwa timu yetu ya Taifa, Taifa stars pamoja na vilabu vya nchini, ni ile sababu ya kutokuthubutu kuwekeza katika soka la vijana ambao ndio kizazi cha kesho.
Msingi wa timu ya taifa hauko kwa akina Nadir Haroub Ally Kanavaro ambao kesho na keshokutwa wanastaafu kucheza soka kwa sababu ya umri wao kuwa mkubwa. Napatwa na mshangao kuona Kanavaro anapotangaza kustaafu mpira watu wengi wakimsikitikia badala ya kumkuza Nickson Kibabage mwenye umri wa miaka 16 kwaajili ya taifa la kesho.
Hatuoni taabu kujiita tunajenga timu itakayokuja kututoa kimasomaso huku tukimtukuza John Bocco ambae kesho na keshokutwa anatundika daruga kwa sababu ya umri wake.
Kama tunataka timu ya kucheza mataifa ya Africa mwaka 2019, hatuna budi kuwakumbatia vijana wa umri chini ya miaka 17 watakaoweza kuwa na uwezo na kuhakikisha katika suala la umri, lakini pia vijana hao wakapewa malezi bora na kutafutiwa mashindano mengi ili kuwatengenezea uzoefu. Timu ya taifa chini ya miaka 17 iliyoenda nchini India kwa mwaliko na kufanya vyema lakini pia kuweza kuwafunga timu ya vijana ya Misri, ule ndio msingi wa kuanzia.
Lakini si ajabu timu ya taifa ya Misri ya vijana iliyofungwa na taifa stars katika mechi ya kirafiki, timu hiyo hiyo ikija baada ya miaka mitano, pengine ikarudisha kisasi cha kufungwa wakiwa watoto.
Katika masuala ya mpira hakuna uchawi ni namna nchi wakishirikiana na shirikisho lenye dhamana ya kusimamia masuala ya mpira ili kuendeleza mashindano kwa vijana kama itakavyokuwa msimu ujao ambapo timu za vijana za vilabu zitakuwa zinacheza kabla ya kupisha mechi za wakubwa.

Hii ndio karata dume, na viongozi wenye dhamana wakisimamia vyema, hakika mashindano ya matifa ya Africa yam waka 2019 yatakuwa yanatuhusu sana nap engine hata kufuzu kwa kombe la dunia la mwaka 2022 itakuwa ni halali yetu. Na ndio maana hata Wales walipotolewa, hawakuwa na sababu ya kusikitika kwani hata hatua ile, kwao ilikuwa ni mafanikio makubwa sana. Tuwatunze, tuwalinde, kwani vijana ni taifa la kesho.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top