
Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya
Tanzania ‘Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa Julai 26, 2016 anatarajia
kutangaza kikosi kwa ajili ya kambi ya awali ya wiki moja ikiwa ni maandalizi
ya kucheza na Nigeria katika mchezo wa kukamilisha ratiba ya kuwania kucheza
fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
Mkwasa amesema lengo la kambi hiyo itakayoanza Agosti mosi, 2016
ni kuwaweka sawa kisaikolojia wachezaji kabla ya kuita kambi nyingine rasmi
wiki ya mwisho ya Agosti kujindaa na mchezo dhidi ya Super Eagles ya Nigeria
unaotarajiwa kuchezwa Lagos Septemba 2, mwaka huu.
Taifa Stars ilipangwa kundi G kuwania kucheza fainali za Kombe
la Mataifa ya Afrika (AFCON) ambazo zitafanyika Gabon, mwaka 2017. Timu
nyingine katika kundi hilo ni Nigeria, Chad na Misri ambayo tayari imefuzu
baada ya kukusanya pointi 10, Nigeria ina pointi mbili.
Taifa Stars mpaka sasa ina pointi moja wakati Chad ikijiitoa
katikati ya mashindano na kukatisha ndoto za Tanzania kucheza fainali hizo.
Post a Comment