
Katika mchezo huo uliomalizika kwa Genk kufungwa bao 2-0,
ilibidi umauliwe kwa mikwaju ya penati baada ya dakika 30 za nyongeza
kumalizika kwa matokeo ya 2-0 yaliyosabaisha matokeo ya jumla kuwa sare ya 2-2.
Ikumbukwe mchezo wa awali (Julai 14) takriban juma moja
lililopita Genk ilipata ushindi wa magoli 2-0 kwenye uwanja wake wa nyumbani
huku Samatta akifunga bao la pili.
Samatta akicheza kwa dakika zote 120, alifunga moja ya penati
ambazo ziliisaidia timu yake kusonga mbele kwenye michuano hiyo. Mikwaju ya
penati kwa upande wa Genk ilifungwa na Dries Wouters, Mbwana
Samatta, Bryan Heynen na Thomas Buffel na kuvusha Genk kwenda raundi ya pili kwa jumla ya penati
4-2.
Genk itapambana na klabu ya Cork City kutoka Jamhuri
ya Ireland katika raundi ya pili ya kutafuta tiketi ya kucheza Europa League
hatua ya makundi.
Post a Comment