
Shirikisho la Soka la Hispania
limemteua Julian Lopetegui kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya nchi hiyo
akichukua nafasi ya Vicente del Bosque.
Del Bosque alijiuzulu wadhifa wake huo kufuatia kutofanya vyema
katika michuano ya Ulaya mwaka huu na sasa Lopetegui, meneja wa zamani wa FC
Porto ndiye atakayeiongoza nchi hiyo kuelekea katika michuano ya Kombe la Dunia
mwaka 2018.
Lopetegui amewahi kuviongoza vikosi cha timu ya taifa ya
Hispania kwa vijana chini ya umri wa 19, 20 na 21, huku akishinda taji la
michuano ya Ulaya akiwa na vikosi vya vijana chini ya umri wa miaka 19 na 21.
Kocha huyo pia amewahi kuiongoza Porto kwa misimu miwili huku
akimaliza katika nafasi ya pili msimu wa 2014-2015 na tatu msimu uliofuata
kabla ya kutimuliwa Januari mwaka huu na nafasi yake kuchukuliwa na Rui Barros.
Lopetegui mwenye umri wa miaka 49, ambaye aliwahi kucheza katika
klabu za Real Madrid na Barcelona akiwa kipa, kibarua chake cha kwanza kitakuwa
mwezi ujao wakati watakapochuana na Ubelgiji katika mchezo wa kimataifa wa
kirafiki.
Post a Comment