Orange imekuwa mdhamini mkuu wa
mashindano makubwa ya CAF kwa miaka minane tangu 2009.
Kabla ya hapo, kampuni nyingine
ya mawasiliano ya MTN ndiyo iliyokuwa mdhamini kwa miaka minne.
Sasa, mdhamini mpya atakuwa
kampuni ya mafuta na gesi ya Total kutoka Ufaransa.
Thamani ya mkataba huo
haijafichuliwa.
Total itakuwa mdhamini mkuu wa:
§
Kombe la Taifa Bingwa
Afrika
§
Ligi ya Klabu Bingwa
Afrika
§
Kombe la Taifa Bingwa
Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN)
§
Super Cup ya Afrika
§
Kombe la Mashirikisho
§
Kombe la Taifa Bingwa
Afrika kwa Wanawake
§
Kombe la Futsal Afrika
§
Kombe la Taifa Bingwa
Afrika wachezaji wa chini ya miaka 23
§
Kombe la Taifa Bingwa
Afrika wachezaji wa chini ya miaka 20
§
Kombe la Taifa Bingwa
Afrika wachezaji wa chini ya miaka 17
Post a Comment