
Waendesha mashtaka wa Afrika Kusini wanasema watakata rufaa kwa mara nyingine tena kupinga hukumu wanayoielezea kama hafifu mno alipopewa Oscar Pistorius ya miaka sita pekee jela kwa kosa la kumuua mpenzi wake mwaka 2013.
Bingwa huyo wa zamani wa mbio za Olimpiki za walemavu, Pistorius mwenye umri wa miaka 29, alihukumiwa miaka 6 jela na jaji Thokozile Masipa baada ya kupatikana na kosa hilo la kuumua Reeva Steenkamp siku ya wapendanao 2013.
Katika rufaa ya awali, alikuwa amekabiliwa na uwezekano wa kufungwa jela zaidi ya miaka 15.
Uamuzi huo ulikuwa umetolewa baada ya kubatilishwa kwa hukumu ya awali ya kuua bila kukusudia wakati jaji huyohuyo Thokozile Masipa alimpa kifungo cha miaka mitano tu jela akisema Pistorius hakukusudia kuua na alidhania amevamiwa na mwizi ndio akafyatua risasi bila kujua ni Reeva Steenkamp aliyekuwa nyuma ya mlango wa bafu.
Hoja hiyo inalopingwa vikali na kambi ya mwendesha mashtaka wakisema Pistorius alijua bayana aliyekuwa akimfatulia risasi ni Reeva kwani walikuwa wote nyumbani kwake siku hiyo ya Valentine, na huenda wapenzi hao walikuwa na ugomvi baina yao .
Upande wa utetezi ulikuwa umesema hawangekata rufaa kwa hukumu hiyo ya pili ya miaka sita.
pande wa mwendesha mashtaka unasema iwapo hawatapigania haki, kwamba Pistorius apewe kifungo kirefu inavyostahili kwa makosa hayo ya mauaji, basi itakuwa mfano mbaya utakaofanya mfumo wa sheria Afrika Kusini udharauliwe.
Wazazi wake Reeva wamesema wanaunga mkono juhudi zote zinazofanywa na waendesha mashtaka kupata haki, na kwamba kifo cha wanawao kimewaathiri vibaya sana kiasi cha kuwasababishia maradhi.
Wanapanga kufungua wakfu kwa jina la mwana wao Reeva aliyekuwa anajulikana sana kama mwanamitindo mwenye sura ya kupendeza.
Post a Comment