Uongozi wa Timu ya Yanga unaendelea na maandalizi kwa
ajili ya safari hiyo. Naye kocha mkuu wa klabu hiyo Mholanzi Hans van Der
Pluijm amesema yupo tayari katika maandalizi makali kwa ajili ya mchezo huo
unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa siku ya Jumanne ijayo, Julai 26, mwaka
huu nchini Ghana.
Yanga itakwenda nchini Ghana ikiwa na kumbukumbu ya
kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 na Medeama Jumamosi iliyopita kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Yanga kwa sasa inashika mkia kwenye Kundi A ikiwa na
pointi moja huku TP Mazembe wakiwa kinara na pointi saba, wakifuatiwa na MO
Bejaia wenye pointi tano.
Post a Comment