
Yanga imeshindwa
kutamba kwa mara nyingine tena kwenye michuano ya kimataifa baada ya kukubali
kipigo cha bao 3-1 mbele ya kwenye mchezo wa Kundi A wa michuano ya
kombe la shirikisho Afrika.
Kikosi cha mholanzi Hans van Pluijm kiliruhusu goli la
mapema lililofungwa dakika ya 7 na Daniel Amoah kabla ya golikipa ya Yanga
Deogratius Muish kudaka mkwaju wa penati uliopigwa na nahodha wa Medeama Paul
Aidoo kufatia Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kumwangusha mchezaji wa Medeama kwenye
eneo la hatari.
Kabla mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania bara
hawajajipanga vizuri wakapigwa goli lingine la pili, safari hii alikuwa ni
Abbas Mohamed aliyepachika bao la hilo baada ya mpira mrefu kumpita mlinzi wa
Yanga Kelvin Yondani na kumkuta mshambuliaji huyo ambaye alimfunga Dida kwa
ufundi.
Mkwaju wa penati uliopigwa na Simon Msuva uliipa Yanga
bao la kwanza na kufanya matokeo kuwa 2-1, penati hiyo ilitokana na Obrey
Chirwa kuangushwa kwenye box la hatari la Medeama.
Abbas Mohamed akaifungia Medeama bao la tatu likiwa ni
bao la pili kwake kwenye mchezo wa leo ambalo liliimaliza Yanga na kuipa mlima
mrefu wa kupanda.
Licha ya Van Pluijm kujaribu kufanya mabadiliko kwa
kumtoa Kelvin Yondani na nafasi yake kuchukuliwa na Vicent Andrew ‘Dante’,
Haruna Niyonzima akampisha Juma Mahadh na nafasi ya Juma Abdul aliyeumia na
kushindwa kuendelea na mchezo ilichukuliwa na Amis Tambwe lakini mabadiko hayo
bado hayakubadilisha matoke.
Matokeo hayo yanaendelea kuiacha Yanga mkiani mwa Kundi A
ikiwa na pointi yake moja baada ya kucheza mechi nne huku TP Mazembe ambayo
itacheza kesho dhidi ya MO Bejaia inaendelea kuongoza Kundi hilo kwa pointi 7
ikifuatiwa na MO Bejaia yenye pointi tano baada ya kucheza michezo mitatu.
Medeama imefikisha pointi tano pia sawa na Bejaia lakini yenyewe imeshacheza
mechi nne mechi moja zaidi ya Bejaia.
Post a Comment