
Mabingwa wa ligi
kuu ya Italia, Juventus wamekamilisha dili lao la kumsajili Gonzalo Higuain
kutoka Napoli kwa ada ya euro mil 90.
Higuain alikuwa akihusishwa kwa muda mrefu kujiunga na
miamba hiyo ya Italy baada ya kukamilisha mazungimzo binafsi mwanzoni mwa mwezi
July.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina (28), amesaini
mkataba wa miaka mitano kwa mabingwa hao wa Serie A walio chini ya Massimiliano
Allegri, ambapo atakuwa akivuta kitita cha euro mil 7 kwa mwaka.
Higuain, ambaye msimu uliopita alifunga mabao 36 kwenye
michezo 35, alijiunga na Napoli mwaka 2013 na kusaini mkataba uliokuwa ukimalizika
June 2018. Sasa ataungana na mastaa wengine kama Miralem Pjanic, Marko Pjaca,
Medhi Benatia na Dani Alves ambao wote wamejiunga na Kibibi kizee hicho cha
Turin kwenye majira haya ya usajili wa kiangazi.
Mbali na Juve
ambao wamefanikiwa kuinasa kandarasi ya mchezaji huyu, Higuain pia alikuwa
ananyatiwa kwa karibu na timu kama vile Arsenal pamoja na Athletical Madrid ya
Nchini Hispania.
Post a Comment