SPORTS

 

Unknown Unknown Author
Title: Lyon Wambania Lacazette Kujiunga na The Gunners.
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya soka Olympique Lyon imekataa ombi la Euro milioni 35 kutoka Arsenal kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette. Mche...
Timu ya soka Olympique Lyon imekataa ombi la Euro milioni 35 kutoka Arsenal kumnunua mshambuliaji wa Ufaransa Alexandre Lacazette.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alifunga mabao 21 katika mechi 34 msimu uliopita na kandarasi yake katika klabu hiyo inakamilika mwaka 2019.
Katika taarifa yake katika mtandao wa Twitter, Klabu hiyo ya Ufaransa ilisema Lacazette hanunuliki na ni miongoni mwa viongozi wa timu hiyo ya kocha Bruno Genesio.
Lyon ilikana ripoti ya gazeti moja kwamba ilikataa ombi la Euro milioni 48 kutoka kwa klabu hiyo ya Uingereza.

Mpaka sasa kocha wa washika bunduki wa London, Mfaransa, Arsene Wenger amekwishakamilisha usajili wa Granit Xshaka na Takuma Asano kinda raia wa Japan.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top