
BAADA ya kuifikia rekodi ya Sir Bobby Charltony
ya mfungaji bora wa muda wote, leo Rooney anaivunja rekodi hiyo na kuandika
rekodi yake baada ya kuifungia United bao la kusawazisha dakika ya 90.
United walikuwa na kibarua kizito kurejesha goli
alilojifunga Mata kipindi cha kwanza.
Sub alizofanya Mourinho, haswa ile ya Mata na
kumuingiza Rooney, ilikuwa na tija baada ya kuisawazishia timu yake goli la
dakika ya 90 na kuipa timu pointi moja.
Lakini kizuri Zaidi ni lile goli la Rooney
ambalo linakuwa goli lake la 250 na hivyo kuwa mfungaji wa muda wote wa United.
Kabla ya
Rooney rekodi hiyo ilikuwa inashikiliwa na Bobby aliyekuwa ana magoli 249.
Rooney bado ana nafasi kubwa sana ya kuendelea kuongeza gap kati yake yeye na
Sir Bobby.
Post a Comment